Verse 1
Mwamba wenye imara, kwako nitajificha
Maji hayo na damu, yaliyo toka humu
Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi
Verse 2
Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria
Nijapofanya bidii, nikilia na kuudhi
Hayaishi makosa, niwe wa kuokoa
Verse 3
Sina cha mkononi, naja msalabani
Nilitupu, nifike, ni mnyonge, nishike
Nilimchafu naja, nioshe nisijafa
Verse 4
Nikungojapo chini, na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini
Roho yangu naiwe, rahani mwako wewe