Mvivu wewe mvivu * 3 mvivu wewe
Hebu watazame wadudu hawa
Hebu watazame sisimizi wewe
Wana adili ya kazi pasipo kusimamiwan(Tazama wanavyojituma (jituma) hawalazimishwi
Tena hawana kiongozi (yeyote) wa kuwapangia)*2n{Ewe mvivu utalala we! we! hatarini
Utaondoka lini katika usingizi wako? }*2
Kwa wenzako kunapokucha, wewe nd'o unalala
Wenzako wanapoamka, wewe wajigeuza
Wenzako wakipanga majukumu, wewe waota ndoto
Wenzako wanapotoka kazini, wewe watupa shuka
Wenzako wanafanya kazi, tena kwa kujituma
Wenzako wanafanya kazi, tena kwa moyo mmoja
Daima wewe wajivuta, tena wingi wa maneno
Hata nazo salamu haziishi, tena sababu mia mia.
Hebu jitazame sasa, umbeya wakutawala,
Tena ukijichunguza, na wizi wakuandama
Wenzako wakifanikiwa, waanza kazi kuwaomba,
Na maisha ya jirani, wewe wayafuatilia
Jiulize utabarikiwa, lini ewe mvivu,
Jiulize utaamka, lini ewe mvivu,
Ukishiba leo huwazi, ya kesho utakula nini
Hakuna lolote ufanyalo bila ya kusimamiwa.