Mungu Yule
{ Nimemuona yule ninayemtafuta na neema zake
Nimemuona -leo nimemuona Mungu } *2n
Mkononi mwake ana uzima tena ni wa milele
Mkononi mwake ana uzima ninaoutafuta
Na uzima huo anatoa bure kwa walio tayari
Lakini kuna kanuni moja ya kwamba, uwajali watu.
Nimemuona Mungu yu mtupu-u hana nguo
Anatamani mimi niende nikamvishe
Nimemuona Mungu ana njaa hana chakula
Anatamani mimi niende nikamlishe
Nimemuona Mungu ni mgonjwa-a kitandani
Anatamani mimi niende kumtazama
Nimemuona Mungu amefungwa-a gerezani
Anatamani mimi niende kumfariji
Nimemuona Mungu ni mkimbizi mpakani
Anatamani mimi niende kumpokea
Nimemuona Mungu ni yatima hana wazazi
Anatamani mimi niende nikamtunze
Nimemuona Mungu ni mjane hana matunzo
Anatamani mimi niende kumhifadhi
Nimemuona Mungu amefiwa ana majonzi
Anatamani mimi niende kumfariji
Nimemuona Mungu ni kilema na hajiwezi
Anatamani mimi niende kumuinua
Nimemuona Mungu atolewa angali mimba
Anatamani mimi niende kumtetea
Nimemuona Mungu anapigwa kwa makombora
Anatamani mimi niende kusuluhisha
Nimemuona Mungu ni mtumwa ananyanyaswa
Anatamani mimi niende kumtetea