Chorus
Nipokee Mungu wangu nipokee *2
Mbele yako ninakuja daima
Sinitupe mbali nawe, mimi mwenye dhambi
Nipokee Mungu wangu wangu nipokee
Verse 2
Adui wako shetani amenizingira, na mitego ya kila aina
Nifanye nini Bwana nisipotee *2
Verse 3
Kila jambo nifanyalo, laenda kombo Bwana
Sijiwezi bila msaada wako, nifanye nini Bwana nikufikie
Verse 4
Mali yangu yote Bwana nitakurudishia
Mimi pia mali yako Bwana, nifanye nini Bwana unipokee
Verse 5
Kwako Bwana nitadumu milele yote Bwana
Na daima nikutumikie, nifanye nini Bwana nifike kwako