SectionsEntranceMungu Wangu Mbona Umeniacha

Mungu Wangu Mbona Umeniacha

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,LentEntrance
Chorus

Mungu wangu mbona umeniacha mimi

Katika taabu zote hizi

Maisha yangu ni ya mashaka

Kwani sina raha nimekosa amani

Matatizo mengi yananisonga (sana)

Nakuomba Bwana nisaidie

Maadui zangu wananiwinda (kutwa)

Wanitega ili wanikamate

Chorus

Ninalala macho wazi mimi (kama ndege)

Kama ndege mkiwa juu ya paa

Nimekuwa kama mhuni mimi (fanya hima)

Fanya hima Bwana kuniokoa

Verse 3

Nimekuwa kama kichekesho kwa watu jamani mimi Bwana

Kila nipitapo hunisema na kunicheka

Wananizushia maneno ya uongo jamani mimi Bwana

Mimi nimekuwa ni jalala la kila baya

Verse 4

Maadui zangu kutwa wanisimanga jamani mimi Bwana

Wananidhihaki wanisonya na kunitusi

Jina langu limekuwa gumzo lao jamani mimi Bwana

Sasa ndilo walitumialo kwa kulaania

Verse 5

Na majivu yamekuwa chakula changu jamani mimi Bwana

Na machozi yangu yamekuwa kinywaji changu

Na siku zangu zinapita kama moshi jamani mimi Bwana

Nakuomba usinichukue bado kijana