SectionsThanksgivingMungu Ni Upendo

Mungu Ni Upendo

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Mungu ni upendo, tupendane *4 ae aen

Tufuateni upendo na kutaka karama za rohoni *2

Lakini zaidi mpate mpate kutubu *2 ae ae

Chorus

{ Nijaposema kwa lugha za wanadamu na malaika

Mimi kama mimi sina upendo - nimekuwa shaba iliayo (mimi)

Nijaposema kwa ndimi za wanadamu na malaika

Mimi kama mimi sina upendo - nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao } *2

Verse 3

Tena nijapokuwa na unabii,

Na kujua siri zote na maarifa yote

Nijapokuwa na imani kamilifu

Kiasi cha kuweza kuhamisha milima

Kama sina upendo, si kitu mimi!

Verse 4

Tena nikitoa mali zangu zote, kuwalisha maskini

Tena nikijitoa mwili wangu, niungue moto

Kama sina upendo, si kitu mimi!

Verse 5

Upendo huvumilia, hufadhili

Upendo hauhusudu, hautakabari

Upendo haujivuni, haujivuni

Verse 6

Haukosi kuwa na adabu

Hautafuti mambo yake

Hauoni uchungu

Hauhesabu mabaya

Haufurahi udhalimu

Bali hufurahi pamoja na ukweli

Huvumilia yote

Huamini yote

Hutumaini yote

Hustahimili yoten

Upendo upendo upendo ni kila kitu