Mungu Baba Pokea
Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary TimePresentation of Gifts
Verse 1
Mungu Baba pokea sadaka yetu leo
Tukutoleayo kwa jina la Mwanao
Ya Abeli na Ibrahimu ilikupendeza
Yetu Baba ipendeze uipokee
Chorus
Ipokee - (ipokee) sadaka yetu
Ndilo fumbo - (ndilo fumbo) la kukupendeza
La Baba na Mwana na Roho Mtakatifu *2
Verse 3
Njooni wote tutoe sadaka yetu leo
Kwa sifa na utukufu wake Mwenyezi
Mkate huu na divai ndivyo mwili wake
Kwa heshima kuu sadaka tumtolee
Verse 4
Ee Mwenyezi tupokee tuwe mali yako
Twakusihi kwa heshima utupokee
Tunakutolea nguvu kazi na mavuno
Kwa huruma yako dhambi tuondolee
Verse 5
Kama mwanzo Mungu Baba a-si-fiwe
Na mwanaye ndiye aliyetukomboa
Roho Mtakatifu ndiye wetu mfariji
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja twakiri