SectionsThanksgivingMungu Awe Nanyi

Mungu Awe Nanyi

Ordinary Time,Pentecostal,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,Wedding,Ordinary Time,WeddingThanksgiving
Chorus

{ Mungu awe nanyi, mshirikiane

Mpate amani katika nyumba yenu } *2

Verse 2

Kushirikiana katika furaha,

Katika uchungu ni matakwa ya Mungu.

Verse 3

Na watoto wenu walee vizuri,

Wamjue Mungu ndiye muumba wao.

Verse 4

Na matendo yenu yampendeze Mungu,

Atawajalia uzima wa milele.

Verse 5

Katika uchungu msaidiane,

Mfarijiane ni matakwa ya Mungu.

Verse 6

Mpatapo shida au matatizo,

Mumuombe Mungu atawasaidia.