Mtume

Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary TimeExit
Verse 1

Dunia hii ni ngumu sana

Yenye mapito mazito

Siku zote watu kulumbana

Kote kote kuna moto

Ooo ni vigumu mno

Ooo kuwajibika

Kwa aliyekutuma

Lakini mimi, tazama

Chorus

Nimeinua macho yangu

Nimtazame mmoja

Yeye ni rafiki yangu

Kisiwa cha faraja

Mimi ni mtume wake

Mtume wa uimbaji

Ninaimba nyimbo zake

Kwa wanaomhitaji Yesu

Verse 3

Duniani kumejaa wivu

Ugombea utukufu

Hasira kali zao wavivu

Watukuzao upofu

Ooo wanaumiza

Ooo wanavunja moyo

Wakatiza tamaa

Lakini mimi, tazama

Verse 4

Duniani kumbe siyo kwangu

Nimetumwa kwa muda tu

Nifanye kazi ya Bwana wangu

Nimalize notoke tu

Ooo nitaitimiza

Ooo nimeamua

Nikavalishwe taji

Milele mimi, tazama

Verse 5

Uchovu usingizi uvivu

Na umaskini wangu

Siruhusu vinitege nyavu

Nishike utume wangu

Ooo ninakaza mwendo

Ooo sirudi nyuma

Sitamwangusha Yesu

Milele mimi tazama

Verse 6

Kwa wanaomhitaji Yesu

Nyimbo zake - kwa wanaomhitaji Yesu

Habari zake - kwa wanaomhitaji Yesu

Na kazi zake - kwa wanaomhitaji Yesu

Mimi nayo nyumba yangu - nitamwimbia Bwana milele

Na waimbaji wenzangu - nitamwimbia Bwana milele

Mimi na rafiki zangu - nitamwimbia Bwana milele

Ndugu na rafiki zangu - nitamwimbia Bwana milele

Nitamwimbia Bwana milelee