SectionsEntranceMtazame Mkombozi Msalabani

Mtazame Mkombozi Msalabani

Ordinary Time,Pentecostal,Ordinary Time,Ordinary Time,EasterEntrance
Chorus

Mtazame Mkombozi msalabani,

Tazama mikono na miguu, vimefungwa kwa misumari

Mtazame Mkombozi msalabani,

Tazama ubavu wake, ulivyochomwa kwa mkuki

Verse 2

Msilie enyi kila mama, msinililieni mimi

Bali watoto wenu, pia nafsi zenu

Verse 3

Mateso gani haya ee Bwana, unayoteseka Mungu wangu

Lipi baya ee Bwana ulilolitenda

Verse 4

Hatia hiyo wanaiunda, hukumuni wanakuingiza

Nawe hujibu neno, wakubali kufa

Verse 5

Nguvu mwilini zimekutoka, mara ya tatu unaanguka

Teso kubwa ee Bwana, lakusonga sana

Verse 6

Juu msalabani unalia, mateso yamezidi sana

Wasema nina kiu, wanakupa siki