SectionsExitMshike Mshike

Mshike Mshike

Ordinary TimeExit
Chorus

{ Hebu wanadamu na tufikirie sasa ni wapi tutakwenda,

Vita vimezidi amani hakuna shetani ametia nanga } *2

Mshike mshike kila kona watu wakimbilia usalama

Lo! Lo! hili jambo limekuwa kawaida

Ona wazee na watoto wateseka

Mshike mshike, mshike mshikenmshikeshike huu utaisha lini?n(Tumuombe Mungu), atikise huu mshikemshike

Verse 2

Ulimwengu wote umekuwa na visa vya ajabu,

Pande moja vita pande nyingine mambo ya ajabu

Tujisitiri wapi, kila pande machungu,

Tunakuomba ee Mwenyezi utupe usalama Baba

Verse 3

Watu nao wamekuwa wakali kuliko wanyama

Tunaishi kama hakuna kizazi kingine tena

Vita vya kila siku, uhasama wa mali,

Kizazi chetu kimekuwa dhiki tena ukiwa sana

Verse 4

Ulimwengu nao umekuwa jeneza la vijana,

Kuvaa vibaya madawa makali wanatumia

Eti wao wajanja, waenda na wakati

Hawajui maisha yana mwisho silaha yao pombe

Verse 5

Hebu fikiria unayefanya mambo haya yote,

Ujue ya kuwa kila lenye mwanzo linao mwisho,

Acha ya kidunia, faida ya ukiwa

Mtegemee Mungu unayo nafasi hii kabla hujafa