SectionsEntranceMpokee Mtumishi Wako

Mpokee Mtumishi Wako

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,LentEntrance
Verse 1

{ Ee Mungu Baba Mwenyezi tuko hapa mbele zako,

Tunakulilia Baba utusikilize } *2

Chorus

Ipokee roho ya mwanao, mpokee mtumishi wako

Mpokee anakuja kwako, mpokee mtumishi wako,

Enyi malaika wa mbinguni, mchukue mpeleke kwa Baba,

Mchukue mpeleke kwa baba

Verse 3

Usiyakumbuke Baba makosa aliyotenda,

Umsamehe makosa ya ujana wake

Verse 4

Fariji roho za wote wanaohuzunika,

Uwape matumaini uwape tulizo

Verse 5

Ee Bwana ungehesabu, makosa ya wanadamu,

Ni nani angesimama mbele yako wewe

Verse 6

Ee Mungu mwenye rehema kumbuka rehema zako

Maana zimekuwapo tokea zamani