SectionsExitMpende Adui

Mpende Adui

Ordinary TimeExit
Verse 1

Bwana Yesu alituachia amri ya mapendo

Ili tupendane kama yeye alivyotupenda

Tena akasema, akasisitiza,

Mpende jirani, kama nafsi yako

Chorus

{ Mpende - adui yako

Mpende - muombee neema

Mpende - adui yako

Mpende - muombee Baraka } *2

Verse 3

Sisi tulivyoumbwa wanadamu hatulingani

Kwa tabia kwa maisha hata kwa matendo yetu

Wapo wa hekima, wasemao ukweli,

Na wenye kiburi, wasio na busara

Verse 4

Hata ukinyanyaswa jitahidi kuvumilia

Usiwe mwenye ghadhabu ukalipiza kisasi

Ukihuzunishwa, mkimbilie Yesu,

Atakupa faraja, heri na fanaka

Verse 5

Usikumbuke ubaya uliokwisha tendewa,

Hiyo itakuwa njia ya kukaribisha chuki

Ukisha samehe, usahau yote,

Ukatae yote, yasiyo ya hekima