SectionsThanksgivingMpendane Daima

Mpendane Daima

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,WeddingThanksgiving
Verse 1

Mungu akaona si vyema mtu huyu awe peke yake

Nitamfanyia mwenzake yule wanafanana naye

Akaumba mwanamke, kamleta kwake mwanamume waishi pamoja

Chorus

{ Ewe Bwana - mpokee mke wako tangu leo

Ewe Bibi - mpokee mume wako tangu leo

Muishi nyote pamoja, mpendane daima

Msitengane daima, msivunje agano } *2

Verse 3

Mungu akawapa uwezo watawale viumbe vyote

Mungu akasema zaeni muijaze dunia kwa watu

Baraka za Mungu Baba, zimewashukia tangu leo zaeni matunda

Verse 4

Ewe mwanamume mpende mke wako kwa moyo wote

Nawe mwanamke heshimu mume wako mtii daima,

Ndoa ni maagano, kati ya watu wawili wapendanao

Verse 5

Nyumba yenu iwe hekalu lake Mungu kanisa ndogo

Nyumba ya amani upole na furaha nyumba ya sala

Mungu ameunganisha mwanadamu asitenganishe daima dawamu