SectionsThanksgivingMoyo Wangu Wa Utulie

Moyo Wangu Wa Utulie

Lent,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus

Moyo wangu na utulie kwako Bwana Mungu wangu - na mwokozi wangu

Maana wewe Bwana ndiwe kimbilio langu - tena mlinzi wangu *2

Chorus

Wewe ndiwe Bwana - wa neema

Fadhili zako - ni za milele

Nikupe nini - Bwana mimi nikushukuru

Umenipa Bwana - na uhai

Pia na nguvu - za kutembea

Nafsi na roho - zangu kweli zimeridhika x2

Verse 3

Asubuhi niamkapo nitalisifu jina lako,

Kwa nyimbo nzuri za furaha mchana mimi nitaimba,

Usiku utimiapo, mimi nitakushukuru,

Kwa maana ninaishi kwa neema zako.

Verse 4

Kila nitembeapo mimi naona utukufu wako,

Wewe waniongoza mimi, kila hatua nipigayo,

Wewe ni Mungu mkuu, na mwenye Baraka tele,

Ninazo sababu tele za kukusifu wewe.

Verse 5

Ewe Bwana unanijua hata ndani ya moyo yangu,

Unaziona siri zangu hata wajua nitakalo,

Ninakuomba ee Bwana, uyajibu maombi yangu,

Kwa kuwa wewe ndiwe tumaini langu

Verse 6

Moyo wangu hukutafuta mchana hata na usiku,

Na mimi ninapokuita kweli wewe huniitika,

Karibu uishi kwangu, nami niwe ndani yako

Usikubali Bwana nitangane na wewe