Chorus
{ Moyo wangu unakutamani,
Moyo wangu unakutamani Mungu wangu } *2n{ Kwa sauti nzuri mimi nikuimbie ee Mungu wangu,
Nitangaze sifa zako milele na hata milele } *2
Verse 2
Nikuambie nini Bwana, ujue ninakupenda
Moyo wangu umekuambia uso wako nitautafuta
Usinifiche uso wako ee Mungu Muumba wangu
Verse 3
Umenitendea mambo mengi, makubwa ya kushangaza
Sasa mimi nitazitangaza fadhili zako Bwana wangu
Asubuhi hata usiku ee Mungu nitakusifu
Verse 4
Nibariki ee Mungu wangu, siku zote za maisha yangu
Nikusifu wewe daima nitangaze uwezo wako
Usiwe mbali Mungu wangu naomba usiniache.