Verse 1
Moyo wako Yesu mpendelevu, watuhurumia maskini
Wawapokelea wakosefu kwa msamaha, wema na amani
Moyo wa hazina ya neema utujalie daima *2
Yesu twasalimu wako moyo, twakushukuru kwa mapenziyo
Verse 2
Moyo makimbilio salama, twakujilia japo wadhambi
Tupokee leo kwa huruma, kasikilize yetu maombi
Yesu uturehemie, kwa wema tufanyizie
Twataka kukutii daima, na kwako kupata usalama *2
Verse 3
Moyo ukashibishwa huzuni, kwa kutustahilia msamaha
Pia ukatiwa msalabani, ya Mbingu utupatie Raha
Tufundishe leo pia kukupenda kuzidia donda lako
Utufungulie kwako milele tukimbilie *2