[ s ] Zikumbukeni njia alizowapitishan[ w ] Amewapenda amewang`ang`ania ninyi
Hajaufumba ukope wake hata mara moja
Amewapenda amewang`ang`ania ninyi
Hajazifumbua mbawa zake msilowe mvua
Amewapenda amewang`ang`ania ah
Lipua pu! pu! pu pu pu! puu!
Lipua sifa - sifa kwa Mungu Baba lipua
Lipua shangwe- sifa kwa Mungu Baba lipua
Lipua tena - sifa kwa Mungu Baba lipua aan(amsheni hisia, lipua sifa, inueni mioyo lipua sifa)
Lipua lipua lipua aa lipua lipua, lipua puu
Kumbuka mlivyokuwa na hali duni kule mwanzo,
Ni yeye Mungu aliyewabeba
Mlipopotea njia akawakamata mkono . . .
Ni yeye Mungu aliyewabeba
Akawaongoza mpaka kufika mlipo leo . . .
Ni yeye Mungu aliyewabeba
[ b ] Kusanyikeni wote kwa miluzi na nyimbo tumtukuze,
Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
Cheza kidogo wote inueni mikono shangilieni.
Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
Rusha miguu yenu kwa midundo mitamu tumtukuze . . .
Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
[ b ] Kusanyikeni wote kwa miluzi na nyimbo tumtukuze,
Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
Cheza kidogo wote inueni mikono shangilieni.
Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
Rusha miguu yenu kwa midundo mitamu tumtukuze . . .
Paza sauti zenu piga kelele kumsifu