Mke Mwema
Ordinary Time,Christmas,WeddingThanksgiving
Chorus
Mke mwema, mke ni nani, awezaye kumuona
Kima chake, kima chapita, kima cha marijanin{Moyo wa mumewe unamwamini,
Wala hatakosa kupata mapato *2}
Verse 2
Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote zote za maisha yake
Verse 3
Hutafuta sufu sufu na kitani,
Taa yake haizimiki usiku
Verse 4
Huwakunjulia maskini mikono,
Huwanyooshea wahitaji mikono
Verse 5
Mwanamke yule amchaye Bwana,
Na huyo ndiye atakayesifiwa
Verse 6
Mpe mapato ya mikono yake,
Basi na kazi yake yamsifu