‘Tukufu! ‘Tukukufu kwa Mungu Juu.
Amani! Na amani duniani
Kwa watu wenye mapenzi - wenyenmapenzi mema x2
A-ma-ni!
Sifa! Sisi tunakusifu
Heshima! Sisi tunakuheshimu
Tunakuabudu - Sisi tunakuabudu. x2
He-shi-ma!
‘Tukufu! Sisi tunakutukuza
Shukrani Sisi tunakushukuru
Kwa ‘jili ya utukufu -
Utukufu wako mkuu x2
Shu-kra-ni!n
Ee Mungu! Ee Bwana Mungu
Ee Baba Mfalme wa mbinguni.
Ee Mungu Baba - Mungu Baba
Mwenyezi x2
Ee Ba-ba!
Ee Bwana! Ee Bwana Yesu Kristu
Ee Mwana Kristu Mwana wa pekee
Mwana wa Baba - Mwanakondoo wa
Mungu x2
Ee Mwa-na!n
Mwokozi Mwenye kuondoa dhambi.
Huruma! Dhambi za dunia
Utuhurumie - Pokea ombi letu x2
Hu-ru-ma!
Ee Yesu Kwani ndiwe Mtakatifu
Ee Kristu Kwani ndiwe Bwana.
Ee Yesu Kristu - Ndiwe peke yako Mkuu! x2
Ee Kri-stu!
Umoja! Pamoja na Roho Mtakatifu.
Milele! Katika utukufu,n‘Tukufu wa Mungu Baba - Kristu anaishi x3
Mi-le-le