Misa Paulo

4 sections

Lord Have Mercy

Lord Have Mercy

Wewe uliyetumwa kuwaponya wanaojuta dhambi

Ee Bwana utuhurumie, ee Bwana utuhurumie

Bwana, Bwana, ee Bwana, ee Bwana utuhurumie

Wewe uliyekuja kuwaita wakosefu

Ee Kristu, utuhurumie, ee Kristu, utuhurumie

Kristu, Kristu, ee Kristu, ee Kristu, utuhurumie

Wewe unayeketi kuume kwa Baba, ukituombea,

Ee Bwana utuhurumie, ee Bwana utuhurumie

Bwana, Bwana, ee Bwana, ee Bwana utuhurumie

Gloria

Glory to God

Chorus

Utukufu (utukufu), utukufu (utukufu),

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

Na amani (na amani) duniani (duniani)

Kwa watu wenye mapenzi mema

Tunakusifu Bwana, tunakuheshimu,

Tunakuabudu (Bwana), tunakutukuza,

Tunakushukuru (tunakushukuru)

Kwa ajili ya utukufu wako mkuu *4

Ee Bwana Mungu, Mfalme wa Mbinguni,

Ee ee Bwana Mungu, Mungu Baba Mwenyezi.

Ee Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee *2

Ee Bwana Mungu, (ee Bwana Mungu)

Mwanakondoo wa Mungu mwana wa Baba *4

Mwenye kuondoa dhambi za dunia,

Utuhurumie, pokea ombi letu

Ee Mwenye kuketi (ee mwenye kuketi)

Kuume kwa Baba tuhurumie *4

Kwa kuwa ndiwe, peke yako Mtakatifu,

Peke yako Bwana Mkuu, peke yako Yesu Kristu

Pamoja na roho (Roho Mtakatifu)

Katika utukufu wa Mungu Baba *4

Holy Holy

Holy, Holy, Holy

{ Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

Bwana Mungu wa majeshi } *2

{ Mbingu na dunia zimejaa,

Utukufu wako Bwana } *2

{ Hosanna juu, Hosanna juu

Hosanna juu, Hosanna juu Mbinguni } *2

{ Mbarikiwa anayekuja, kwa jina la Bwana } *2

Lamb of God

Agnus Dei

Mwanakondoo, ee Mwanakondoo

Ee Mwanakondoo wa Mungu

Uondoaye dhambi za dunia,n{ Utuhurumie, utuhurumie } *2 huruma!

Mwanakondoo, ee Mwanakondoo

Ee Mwanakondoo wa Mungu

Uondoaye dhambi za dunia,n{ Utuhurumie, utuhurumie } *2 huruma!

Mwanakondoo, ee Mwanakondoo

Ee Mwanakondoo wa Mungu

Uondoaye dhambi za dunia,n{ Utujalie amani } *2 amani