SectionsEucharistMisa Kariobangi (Nasadiki)

Misa Kariobangi (Nasadiki)

Ordinary Time,MarianEucharist
Verse 1

Nasadiki kwa Mungu mmoja -

Ndiye Baba yetu Mwenyezi -

Mwumba mbingu pia dunia -

Nasadiki kwa Yesu Kristu -

Chorus

Nasadiki, nasadiki, ninasadiki,

Nasadiki, nasadiki, ninasadiki.

Verse 3

Mwana wa pekee wa Mungu -

Mwenye kuzaliwa kwa Baba -

Akapata mwili kwa Roho -n‘Kazaliwa naye Bikira -

Verse 4

Kisha yeye ‘kasulibiwa -

Kwa amri ya Ponsyo Pilato -Kwa ajili yetu kateswa -

Akafa na akazikwa -

Verse 5

‘Kafufuka katika wafu -n‘Kapaa juu mbinguni -

Ameketi kuume kwake -

Mungu Baba yetu Mwenyezi -

Verse 6

Ndipo atakapotokea -

Kuhukumu wazima na wafu -

Kwake Roho Mtakatifu -

Kwa kanisa la Katoliki -

Verse 7

Ushirika wa watakatifu -n‘Ondoleo ya dhambi -

Nangojea ufufuko wa mwili -

Na uzima wa milele -n