Verse 1
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni,
Na amani iwe kwa watu wenye
Mapenzi mema duniani kote.
Chorus
Tunakusifu,
Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu,ntunakutukuza.
Verse 3
Tunakushukuru, Mungu kwa ajili,
Ya ‘tukufu wako mkuu, ee Bwana, ni
Mungu ndiwe Mfalme wa mbinguni
Verse 4
Ee Baba Mwenyezi, Bwana Yesu Kristu,
Ee Mwana wa pekee, ee Mungu Mwana
Kondoo wa Mungu, Mwana wake Baba.
Verse 5
Mwenye kuondoa dhambi za dunia,
Utuhurumie, ‘tuhurumie,
Maombi yetu, Bwana, uyapokee.
Mwenye kuketi kuume kwa Baba,
Verse 6
Utuhurumie, kwa kuwa ndiwe
Pekee yako ni Mtakatifu
Verse 7
Pekee yako, Bwana, pekee yako mkuu,
Ewe Yesu Kristu, pamoja naye
Roho Mtakatifu milele yote.