Chorus
{ Mimi ni mtumishi wake Bwana, nitendewe ulivyonena *2
Nitendewe ulivyonena, mimi ni mtumishi wa Bwana } *3
Verse 2
Salamu uliyejaa neema, Bwana yu pamoja nawe
Usiogope Maria, Mungu kakupendelea
Verse 3
Tazama utapata mimba utazaa mwana, utamwita jina Yesu,
Huyu atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa aliye juu
Verse 4
Bwana Mungu atampa kiti cha enzi, cha Baba yeke Daudi
Ataitawala nyumba ya Yakobo hata milele
Ufalme wake hautakuwa na mwisho