{Mimi ndimi Baba yao Baba milele (milele),nnao ni wanangu Nitawasikiliza nitasikia (mimi),nwakinililia katika taabu} *2
Mimi ndimi wokovu wa watu, nitawaokoa
Wakinililia katika taabu yoyote, nitawasikia
Mimi ndimi aishikaye kweli, nitawahukumu
Walioonewa na taifa lisilo haki, nitawafungua
Mimi ndimi mchungaji mwe-ema, nitawakusanya
Waliotawanyikia nchi za ugenini, nitawarejesha
Mimi ndimi mwa-limu wa watu, nitawafundisha
Waliolemewa na mizigo yao mizito, nitawapumzisha
Mimi ndimi m-kate wa uzima, nitawashibisha
Wote wenye njaa na kiu ya haki hakika, nitawashibisha
Mimi ndimi ufufuo wa kweli, nitawafufua
Wakinirudia na kutubu maasi yao, nitawasamehe
Mimi ndimi kimbilio la watu, nitawahifadhi
Waliotengwa kando na jamaa zao, nitawapokea
Mi-mi ndimi wo-kovu wa watu, nitawaokoa
Wakinililia katika taabu yoyote, nitawasikia