Chorus
[s] Mimi mzabibu wa kweli, mimi mzabibu wa kweli,
Nanyi m matawi yangu, Baba yangu ni mkulima,
Mwenye kutunza shamba lake } *2n[s] Tawi lile lisilozaa
Baba yangu huliondoa, na kuliteketeza moto,n[s] Tawi lile linalozaa
Baba yangu hulisafisha, lidumu katika kuzaa
Hayo - hayo ni maneno ya Bwana Yesu }*2
Verse 2
Nyinyi mmekwisha, kuwa wasafi,
Kwa sababu ya neno, nililowaambia
Kaeni nami, ndani yangu,
Na mimi na mimi na mimi ndani yenu
Verse 3
Akaaye ndani yangu, huyo atazaa
Kwani nje yangu, hataweza kuzaa
Kama vile nje ya mzabibu,
Tawi halitaweza kamwe kuzaa.
Verse 4
Maneno yangu yakikaa ndani mwenu,
Ombeni lolote mtatendewa
Naye Baba yangu atatukuzwa,
Na nyinyi mtakuwa wanafunzi wangu