Chorus
{ Sasa ni wakati mwafaka wa kutoa sadaka yako ndugu
Hima ndugu jitolee kwa moyo wa ukarimu } *2
Iwe ni fedha pia hata mali umtolee Muumba wako
Akulindaye akuamshaye akupaye hewa na afya njeman{ Waumini, wote tuamke pamoja na sasa tujenge kanisa
Kanisa letu litasitawi kwa michango michango yetu } *2
Verse 2
Kwa moyo wako wa ukarimu mpe muumba wako
Sadaka yako kama shukrani yako
Ujiulize kwa jinsi gani, Bwana kakubariki
Umtolee kama shukrani yako.
Verse 3
Wiki hii nzima amekulinda sasa jifikirie
Ni kitu gani kiwe dhamana yako
Umshukuru kwa jinsi gani naye afurahie
Kwa mema mengi anayotenda kwangu,
Verse 4
Wewe mzima ni wengi sana leo hawaamki
Jifikirie ni wangapi umetenga
Na familia yako daima shida haziwakumbi
Si kwamba hao ni bora kuliko wote.