SectionsEntranceMfalme Wa Amani

Mfalme Wa Amani

Ordinary Time,EasterEntrance
Verse 1

Mfalme wa amani mpeni heshima,

Yerusalem mjini anaingia

Na unyenyekeo na upole mkuu

Anapanda punda Mwana wa Mungu.

Chorus

Hosana juu, hosana Juu, hosana juu.

Verse 3

Njooni Mahebruni, njooni watoto,

Leteni matawi ya kumsalimu.

Mwana wa Daudi kweli Masiya

Anakuja kwenu mwenye huruma.

Verse 4

Tandikeni nguo miguuni pake,

Imbeni zaburi, shangilieni.

Mbarikiwa huyu ajaye kwetu

Kwa Jina la Bwana Mkombozi mkuu.

Verse 5

Ufurahi sana, we` Yerusalem

Yule wamwabudu roho za mbingu.

Na huruma pale anakujia,

Haki na amani akuletea.

Verse 6

Ndimi za wachanga zafumbulia,

Kwa mwujiza sifa yake Masiya

Na makundi yote ya malaika

Sifa na heshima wanamtolea.