SectionsExitMchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio

Mchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio

Ordinary TimeExit
Verse 1

La mgambo sasa limelia tembea ndugu yangu tena ukaze mwendo

Safari yetu bado ni ndefu tushikane tutembee pamoja

Milima pia nayo mabonde, tazama visije kuwa ni vikwazo kwako

Ubebapo Neno lake Mungu songa mbele usirudi nyuma

Chorus

{Hima hima twendeni kwa pamoja

Mchaka mchaka twendeni mbio mbionaee iye ye he he he hehenaee iye ye he he he iye

Twendeni wote mbinguni kwa Baba} *2

Verse 3

Watu wengi wana mali nyingi lakini kutoa sadaka kwao ni ndoto

Wengi wao bila kuogopa humpa Mungu wao chenji

Wengine huwatesa wajane jamani tena kuwanyanyapaa yatima

Ikiwa unaitamani mbingu tenda wema na twende pamoja

Verse 4

Tuzingatie tabia yako nao wale wenzetu pia tuwasaidie

Badala ya kusubiri wafe na kutazama kwenye misiba

Kumbukeni maneno ya Yesu aliyonena kupitia Injili Luka

Mimi nilipokuwa mgonjwa hamkuja kunitazama

Verse 5

Wengine wamekataa toba husema siwezi kutubu kwa mwanadamu

Wamesahau ya kwamba Mungu alituachia makasisi

Amewapatia mamlaka hakika watakalolifunga duniani

Na mbinguni pia itafungwa ole wenu mnaowadharau