SectionsExitMbona Nahangaika

Mbona Nahangaika

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,LentExit
Chorus

{ Mbona nahangaika, mkiwa mimi,

Sina hata wa kunifuta machozi } *2

Ni aibu gani iliyonitanda,

Najuta hata siku ya kuzaliwa kwangun{ Maskini mimi, nitakuwa mgeni wa nani,

Nakulilia e Mungu uniokoe } *2

Verse 2

Taabu na matatizo yanisonga mimi

Shida nazo karaha zanisumbua mimi,

Mungu ufanye hima uniokoe.

Verse 3

Nimeugua nikilalama, mnyonge mimi,

Sina rafiki wala mtetezi, mkiwa mimi

Wote wamenigeuka kuniwinda,

Verse 4

Kila waliwazalo juu yangu ni baya,

Kuugua kwangu kumbe ni furaha kwao

Walitaka nife nisahaulike.