Verse 1
Mbona mwafurahi, (leo) sisi tuna amani (kweli)
Mbona mwafurahi, (leo) sisi tuna upendo (kweli)
Chorus
{ Yesu ni mwalimu (kweli), tena ni dereva (wetu)
Akiwa usukani sisi tuko salama } *2
Verse 3
M-nakwenda wapi, (kule) nyumbani mwake Bwana
Leo kuna nini, (ili) tutoe shukrani (zetu)
Verse 4
Njooni watu wote, (leo) tukamwimbie Mungu
Njooni tusujudu, (humu) hekaluni- mwake
Verse 5
Mwili wake Bwana, (ni) chakula cha roho (zetu)
Damu yake Bwana, (ni) kinywaji cha- kweli (kweli)
Verse 6
Tufanyeni shangwe, viumbe wake Mungu (Baba)
Kwa vigelegele, (pia) kwa kupiga makofi (sana)