Chorus
Mlipokea nguvu ya Mungu ya kushinda tamaa
Siku ile mlipobatizwa,
Mkaahidi kumkataa, Ibilisi na vyake,
Sasa vipi muwe wabinafsi
Hamshibishwi kwa riziki yenu,
Aliyowapimia Mungu wenu
Mnatafuna riziki ya hao walio wadogo
Mnakula rushwa ndugu zangu
Verse 2
Uhai na nguvu mlivyojaliwa, si kwa ajili yenu,
Ni kwa ajili ya wahitaji
Verse 3
Elimu mliyoipata wapendwa, si utukufu wenu
Akatukuzwe Muumba wenu
Verse 4
Fedha navyo vyeo mlivyoazimwa
Jembe la Mungu wenu, mkatumikie shamba lake
Verse 5
Acheni umimi acheni ulafi, ingawa kuna leo
Kumbuka kwamba na kesho ipo
Verse 6
Kipimo mnachowawia wadogo, hicho kitatumika
Usoni penu siku ya mwisho