SectionsExitMbinguni Ni Furaha

Mbinguni Ni Furaha

Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Verse 1

Nimeahidiwa utukufu mbinguni – Kwake Mungu Baba

Nikamilishapo kazi yake Bwana – Aliyeniumba

Nitatunukiwa tuzo za kifalme – nikiwa mshindi

Chorus

{t/b} Mbinguni ni furaha

Tutaimba, na kucheza

Tutaruka kwa furaha tukimwona Mungu,

Tuendapo paradiso aliyotuandalia sisi wateule x2

Verse 3

Nyimbo za ushindi mimi nitaimba – Nikimwona Mungu

Sauti za mbinguni mimi nitapewa – naye Mungu wangu

Nikiwa na kwaya tamu za malaika – wote wa mbinguni

Tutaimba hosanna

Verse 4

Makao ya kifahari mimi nitapewa – nilioandaliwa

Yaliyo na urembo usio na mifano – ya dhamani kubwa

Mandhari ya dhahabu na pia almasi – yanayometemeta

Mbinguni kwapendeza.

Verse 5

Nitashangilia nikiwa barazani – pamoja na Mungu

Na watakatifu wake Mungu Baba – walionitangulia

Karamu ya wateule tutaandaliwa – kufutwa machozi,

Kwa shangwe na nderemo.

Verse 6

Makao ya kifahari kweli ni mazuri – tena matulivu,

Yasiyo na njaa shida wala kifo – furaha kila siku,

Kazi ni kumsifu na kutukuza Mungu – milele amina

Huko ndiko nyumbani.