SectionsExitMbinguni Kutakuwa Raha

Mbinguni Kutakuwa Raha

Ordinary TimeExit
Chorus

Nakiri kuwasimulieni na kuwapa siri hii hakika

Mbinguni kutakuwa raha kwa wale wote watakaofika

Hili jambo labidi nitamke kwani nimefikiria hakika

Hakutakuwa rushwa hongo, hirizi wala mlango wa kona,n

Heri waliochaguliwa kufurahi na Mwanakondoo

Waliovumilia shida, starehe na anasa za nchin

Ole wenu (ole), ole wenu (ole) ole wenu mnaocheka sasa

Mtalia (nyinyi) mtalia (nyinyi) mtalia na kuomboleza

Ole wenu (ole) Ole wenu (ole) ole wenu mpiganao sasa

Fainali yake inakuja mshahara ni mauti

Verse 2

Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao rushwa

Siku zinakuja nayo rushwa pia itakuhukumu

Verse 3

Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao wizi

Siku zinakuja vyote ulivyoiba utarudisha

Verse 4

Furahini furahini nyinyi mpendao haki

Siku zinakuja mtakuwa wakuu wa wafalme

Verse 5

Furahini furahini mtesekao kwa dhiki

Siku zinakuja ufalme wote utakuwa ni wenu