SectionsThanksgivingMataifa Yote Ya Ulimwengu

Mataifa Yote Ya Ulimwengu

Thanksgiving
Chorus

Mataifa yote ya ulimwengu

Yatakusujudia ee Mungu (Mungu Baba) *2

Mema uliyonitendea Mungu wangu ninashukuru

Jana leo nimeamka kesho sijui itakuwa vipi

Ninashukuru mungu wangu leo

Na kwa nyimbo nzuri naimba ili

Kesho nayo niwe salama

Nazo sifa zako nitangaze pote *2n

Verse 2

Uamkapo asubuhi ndugu yangu

Ushukuru Mungu

Kwa jinsi alivyokulinda

Usiku kwenye giza tororo

Uimbe kwa furaha na

Kuchezacheza kwa madaha

Verse 3

Ufikapo safari yako ndugu yangu

Umshukuru Mungu,

Kwa jinsi alivyokulinda

Na ajali za barabarani

Uimbe kwa furaha na

Kuchezacheza kwa madahan

Verse 4

Shikaneni mikono sasa

Yote muinyanyue juu

Semeni kwa shangwe na mbwembwe

Maneno haya kwa furaha

Ameweza Bwana Mungu

Kweli ameweza amewezan

Verse 5

Akina mama simameni sasa

Mpige vigelegele

Na kina Baba nyanyukeni

Mpige makofi kwa shangwe

Muimbe kwa furaha na

Kuchezacheza kwa madaha