Mataifa Ya Ulimwengu
{ Mataifa yote ya ulimwengu
Yatakusujudia ee Mungu (Mungu Baba) } *2n{ Mema uliyonitendea Mungu wangu ninashukuru
Jana leo nimeamka kesho sijui itakuwa vipi
Ninashukuru Mungu wangu leo
Na nyimbo nzuri ninaimba ili kesho nayo niwe salama
Nazo sifa zako, nitangaze pote } *2
Uamkapo asubuhi ndugu yangu, umshukuru Mungu
Kwa jinsi alivyokulinda usiku wenye giza tororo
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha
Ufikapo safari yako ndugu yangu, umshukuru Mungu
Kwa jinsi alivyokulinda na ajali za barabarani
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha
Shikaneni mikono sasa yote muinyanyue juu
Semeni kwa shangwe na mbwebwe maneno haya kwa furaha
Ameweza Bwana Mungu kweli ameweza ameweza
Akina mama simameni sasa mpige vigelegele
Na kina Baba nyanyukeni mpige makofi ya shangwe
Muimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha