Maneno

Ordinary Time,Ordinary TimeBible Procession
Verse 1

Tazama nimesikia nimesikia mahusia yako,

Tazama nimeelewa nimeelewa maagizo yako

Ee Bwana nimevutiwa, nimevutiwa nayo njia yako

Ee Bwana nimeamua kuyapokea mafundisho yako

Tazama nimesikia tazama mahusia tazama nimesikia na nimeelewa

Na ninainuka sasa ninakuja

Chorus

{ Natembea kwa imani ninakuja hapo ulipo

Tena kwa matumaini ninakuja hapo ulipo

Uyaweke maneno maneno yako kinyani mwangu

Nikahubiri maneno yako kwa ulimwengu } *2

Verse 3

Nakumbuka ulivyoahidi kuwa nami kila mahali

Na kunifundisha lugha nitakayoizungumza

Tena utakavyonipa nguvu barazani mwa watawala

Watakapotaka kunihukumu kusudi waufiche ukweli

Verse 4

Tena umenitahadharisha nitapigwa na maadui

Kama kondoo kati ya mbwa mwitu nitavamiwa

Naomba neema yako Bwana ili nisikate tamaa

Ujumbe wangu niufikishe kwa watu bila kuvunjika moyo

Verse 5

Haya yote yakakupe wewe utukufu sifa heshima

Utukuzwe Mungu Baba Mwana na Roho Mtakatifu

Kama vile vile ilivyokuwa mwanzo na ilivyo sasa

Utukuzwe vivyo hivyo Mungu daima hata milele milele

Verse 6

< hitimisho >

Maneno maneno yako kinywani mwangu

Hubiri maneno yako kwa ulimwengu

Uyaweke maneno yako kinywani mwangu

Niende nikahubiri maneno yako kwa watu wote