SectionsEntranceManeno Ya Saba Ya Yesu Msalabani

Maneno Ya Saba Ya Yesu Msalabani

Marian,LentEntrance
Verse 1

Baada ya kuteswa na kusulubiwshwa msalabani

Aliona walichokifanya hawakukijua

Aliwaombea kwa Mungu akisema

Baba uwasamehe hawalijui wanalofanya

Verse 2

Kulikuwa mhalifu liyemtambua kuwa yeye ni Mungu

Alitubu akaambiwa

Nakuambia hakika leo, utakuwa pamoja nami peponi

Verse 3

Alitukabidhi kwa mama yake

Na huyo ndiyo mwombezi wetu aliposema

Mama tazama huyu ndiye mwanao

Tazama huyu ndiye mamako

Verse 4

Aliona kiu baada ya mateso makali

Hadi alisema mwenyewe naona kiu

Verse 5

Baada ya mateso makali hayo

Aliyoteswa kwa ajili ya dhambi zetu

Aliona yote aliyotumwa na Mungu kuwa yametimia

Aliposema Yametimia *2

Verse 6

Ndipo alipolia kwa uchungu na kumbwambia Baba

Eloi eloi lamasabakidani, Mungu wangu Mbona umeniacha

Verse 7

Mwisho kabisa aliikabidhi roho yake kwa Baba

Akisema Baba mikononi mwako Naiweka Roho yangu