SectionsExitManeno Tu

Maneno Tu

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Hohohohoho maneno hohohohoho maneno tu *2

Hoo hoo maneno ohoo bila matendo x2

Nampenda Mungu ( maneno tu )

Nampenda Mungu (maneno tu) hayooooo

Verse 2

Kutwa kucha maneno tu familia yako inayumba amani imetoweka hiyo..

Umeitelekeza unaponda mali kwa anasa huna wasiwasi,

Umeiangamiza unaponda mali weee- eti nampenda Mungu eeh, ehee, maneno tu

Verse 3

Kutwa kucha maneno tu hupatani na jirani yako hata salamu hampeani,

Matatizo yake wayashabikia kwa furaha huna wasiwasi,

Nazo shida zake wazishangilia weee - eti nampenda Mungu eeh,ehee,maneno tu

Verse 4

Kutwa kucha maneno tu madaraka yako ni ya uma, unayafuja unavyopenda,

Hauwajali watu wanaoteseka waliao huna wasiwasi

Hauwajali watu wanaoumia weee - eti nampenda Mungu eeh,ehee,maneno tu

Verse 5

Tena nampenda Mungu wangu- nampenda nampenda kuliko kitu chochote

Na jirani yangu nampenda- nampenda kama nafsi yangu.

Ni amri ya Mungu( tena) ndiyo amri kuu,nlakini matendo yako hayafanani na maneno,nunang'ara uso wako, moyoni unang'ata meno,

Tazama, matendo, matendo yako, tazama mwenendo, mwenendo wako( aiyooo)

Ndugu acha maneno,( ooh hayoo) maneno tu,

Upendo ni matendo (na kabisa ni) matendo

Ndugu acha maneno (ooh acha) maneno tu,

Upendo ni matendo ( na kabisa ni ) matendo *2