Mambo Ya Yesu

Ordinary TimeBible Procession
Chorus

{ Hatutaacha kuyanena mambo ya Yesu

Hatutaacha kuyasimulia matendo yake Kristu } *2n(Sisi) uliyoyaona na kuyasikia wenyewe (Yesu)

Akimwaga damu yake msalabani tukombolewe

Tuliyoyaona na kuyasikia wenyewe (hivyo)

Maisha yangu na uhai wangu mimi namkabidhi Yesu

Verse 2

Amewaponya wenye magonjwa wakawa huru

Akawafufua wafu nao wakawa hai

Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu

Verse 3

Alitoa uhai wake kwa ajili yetu

Akafa kifo cha aibu pale msalabani

Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu

Verse 4

Ametuachia karamu iliyo kuu,

Karamu ya upatanisho nay a upendo

Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu

Verse 5

Alibadilisha maji yakawa divai

Na wenye harusi wakanywa wakafurahi

Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu