SectionsExitMama Akaitika

Mama Akaitika

Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Easter,Wedding,Wedding,Christmas,Ordinary Time,Wedding,Easter,Lent,Ordinary Time,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Christmas,Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Hatari ikaja nikageuka mbio kumlilia -

Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee

Akaifungua mikono yake myema kanidaka -

Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee

Nikalaza kichwa kifuani kwa mama nikihema-

Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee

Chorus

|t| Mama anayenipenda, Maria ananijali,

Popote ninapokwenda, mimi niko salama,

Nitakimbilia hapo hapo kwa mama wa

Nitakimbilia hapo hapo kwa mama wa upendon

Chorus

|w| Mama yangu Maria nyumba ya salama

Mama yangu Maria nyumba ya salama

A hapo hapo kwa mama wa upendo

Ni hapo hapo kwa mama wa upendo

Verse 4

Wenye nguvu zao walibeba silaha, kupigana -

Wakapigania ndani ya nyumba yetu, hatari kuu

Wakazidiana paa wakalipua,tumekwisha -

Verse 5

Kwenye familia migogoro ya ndoa shida tupu -

Watoto wakawa na maadili duni, balaa tu -

Na magonjwa lundo uchumi hohehahe, taabu tu

Verse 6

Bibi yangu Eva alizaa laana duniani -

Mama yangu mwema akazaa wokovu,wa milele

Nkakabidhiwa niwe mwanaye naye, mamangu ee -

Verse 7

Uovu wa watu ulishika hatamu kila kona -

Amani ikawa ndoto ya jua kali haipo ee -

Hofu na mashaka vikafunika nchi,hatari kuu -

Verse 8

Baba wa kanisa akaniita shime tujiunge-

Tusali rozari tumlilie mama wa amani -

Atatusikia ataushusha mkono wa Yesu -