Matumaini ya safari yetu, sasa yameingia dosari
Kwani meli tuliyopanda, kuja kwako,
Tazama imevamiwa na majambazi
Hatuna njia nyingine itakayotuokoa kwenye janga hili
Yesu mwema njoo haraka, utuokoe wanao tunakwisha wote
Gonjwa hatari, lisilotibika, ona linatumaliza wote
Halichagui halibagui, linafyeka,
Ukimwi, halina huruma kwa wanadamu
Limeua watu wengi, ni wengi wakubwa kwa wadogo wamepotea
Milenia tuliyomaliza, ilijaa huzuni na majonzi kila upande
Wanasayansi madaktari, wanaahangaika kutwa kucha
Juhudi zinagonga mwamba, hakuna dawa
Ee Bwana tunakufa tuonee huruma
Tunaomba Mungu Mwenyezi, ingilia katika uwezo wako wote
Macho yao uyafumbue, fanaka ipatikane, Bwana tunakuomba
Tumeshaomba, tumesali sana, ee Bwana sikia sala zetu
Tunaungama tumekosa Mungu Mwenyezi,ntazama, Tunakulilia tusikilize
Tunakufa kama nzige, ee Mungu ee Bwana tunateketea wote
Si Sodoma wala Gomora, jamani hili linazidi tena latisha
Ee Yesu Mwema, mwenye huruma, tunakuomba ututazame
Damu na maji vilivyotoka mwilini mwako
Zilete dawa halisi ya kutuponya
Watoto ni wengi sana wanakufa bila ya hatia, inasikitisha
Wengine sasa ni yatima, hawajui wataishi vipi maisha yao
Tunakuomba, ee Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu
Milenia tuliyoianza, njoo Bwana,
Haraka ukatawale mioyo yetu
Machozi tunayolia yafute maovu yetu yote kwa neema yako
Lakini mapenzi yako yatimizwe vile utakavyotuashiria