SectionsEntranceLo Kaburi Wazi

Lo Kaburi Wazi

Wedding,Ordinary Time,Easter,Christmas,Christmas,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Lent,EasterEntrance
Verse 1

Mama Maria tuambie, uliona nini njiani

Nanyi mitume tueleze mliyemkuta pangonin{ (kweli) Ni malaika, toka mbinguni

Tulimwona pale kaburini } *2

Chorus

Lo! Kaburi wazi!

Hayumo, ni mzima, hayumo, amefufuka *2

Lo! Kashinda kifo!

Mauti, yameshindwa, tuimbe, tushangilie *2

Verse 3

Amefufuka ni hakika, amefufuka kweli kweli

Dunia nzima ifurahi, hata mbinguni wanaimban{ (kweli) Twimbe tucheze, twimbe turuke,

Twimbe sana , twimbe aleluya } *2

Verse 4

Nguvu za shetani kashinda, kamba za mauti amekata

Ngome ya kuzimu kavunja, kaburi za wafu zafungukan{ (kweli) Simba wa Yuda, amenguruma,

Walinzi nao mbio watimua } *2

Verse 5

Ameondoka kaburini, aelekea Galilaya

Nasi twendeni hima hima, twendeni kule Galilayan{ (kweli) Twendeni leo, twendeni sote,

Tumwimbie nyimbo za ushindi } *2

Verse 6

Tumekombolewa kwa damu, damu yake Mwanakondoo

Lango la mbingu liko wazi, kwao waliokombolewan{ (kweli) Tukimwamini, tutaingia,

Tutaishi na Mungu milele } *2