SectionsThanksgivingLo Ajabu Kupata Uzima

Lo Ajabu Kupata Uzima

Wedding,Ordinary Time,Easter,Christmas,Christmas,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,LentThanksgiving
Verse 1

Lo! Ajabu kupata uzima,

Katika damu ya Mwokozi wangu

Aliyenifia pendoni

Mimi niliyemsulubisha

Upendo huu wa kushangaza kabisa

Wewe Yesu wangu kunifia pendoni

Chorus

{ Upe - upendo huu,

Nashaa- nashangaa,

Yesu - Yesu wangu kunifilia } * 2

Verse 3

Yesu wangu alitoa damu

Siwezi kuelewa neno hili

Viumbe vyote vya Mbinguni

Navyo haviwezi kufahamu

Najua tu ni kwa rehema zake Mungu

Malaika watu wote wamsujudu mno

Chorus

{ Ni re - ni rehema

Tumwa - tumwabudu

Tumwa - tumwamini ndiye Mwokozi } * 2

Verse 5

Aliondoka kule mbinguni

Kwa nyumba yake Mungu Baba yake

Na utukufu aliacha

Afe kwa ajili ya maovu

Rehema zake ni nyingi na ukarimu

Kwani Mungu wangu aliniokoa mimi

Chorus

{ Sista - sistahili

Neema - neema zake

Laki - lakini alinioka } * 2

Verse 7

Roho yangu ilifungwa sana

Dhambi na giza vilinilemea

Akaniangaza rohoni

Gereza langu likang'aa mno

Ikafunguka minyororo yangu yote

Nikaondoka nikaanza kumfuata

Chorus

{ Siku - siku ile

Nika - nikapata

Uhu - uhuru kweli kwake Mungu } * 2

Verse 9

Hukumuni mimi simo sasa

Mimi ni wake Yesu ndiye wangu

Yeye ni kichwa changu kweli

Na amenivika haki yake

Mimi hodari sasa kwa kiti cha enzi

Napewa taji ya milele katika Yesu

Chorus

{ Sina - sina hofu

Kuso - kusogea

Kati - katika Bwana wangu Kristo } * 2