Litukuzeni Jina
Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Wedding,Easter,Wedding,Wedding,Christmas,Ordinary Time,Wedding,Easter,Lent,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1
Litukuzeni Jina la Mungu daima milele
Enyi mataifa, mshangilieni Mungu wetu
Kwa kuwa Bwana ni Mtukufu wa kutisha
Yeye ni mfalme mkuu wa dunia yote
Sifuni Bwana kwa shangwe
Chorus
{Jina la Mungu lihimidiwe daima milelen( litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe)
Enyi mataifa mhimidini
Kwa kuwa fadhili zake (kwetu sisi) zadumu daima milele } *2
Verse 3
Jina lake Bwana litukuzwe sasa hata milele
Viumbe vya Bwana Sifuni Bwana Mungu wetu
Toka mawio hata machweo ya jua
Sifuni jina lake Bwana Mungu wetu
Sifuni Bwana Mwenyezi
Verse 4
Enyi watumishi sifuni Bwana kutoka Mbinguni
Mbingu nanyi maji, lisifuni jina la Bwana
Wafalme wa dunia nanyi watu wote
Wakuu nanyi wakaazi wote wa dunia
Sifuni Bwana Mwenyezi