Verse 1
Leo Yesu kazaliwa, wakristu twashangilia
Habari njema kwa Wakristu, kokote washangilia
Amezaliwa Mkombozi, atuokoe dhambini
Mwokozi amezaliwa
Chorus
Njooni tumshangilie leo amezaliwa
Aliyetabiriwa Mowokozi amezaliwa
Ameacha enzi yake ili aje kutuokoa*2
Verse 3
Malaika wa Mbinguni wanaimba aleluya
Furaha kote duniani Wakristu wanashangilia
Mwangaza kote duniani, Wakristu wameupata
Mwokozi amezaliwa
Verse 4
Azaliwe ndani yetu, ndilo tumaini letu
Tukimwamini Yesu Kristu, azaliwe ndani yetu
Tutaupata uzima alioleta uzima
Mwokozi amezaliwa