Verse 1
Kwa nyimbo nzuri za furaha,nnjooni nyote mbele za Bwana
Kwa shangwe na vigelegele,ntumwimbie Mfalme wetu
Chorus
Mataifa yote simameni mbele zake Bwana,
Makabila yote njoni leo nazo ngoma zenu
Chezeni mbele za Bwana!n{ Wajaluo na waimbe nyimbo
Wamasai na waruke juu
Wabaluhyia na wapige ngoma
Wakikuyu na wacheze sana,
Watu wote sisimukeni,
Shangwe nderemo na kelele, pigeni makofi } *2
Verse 3
Vinanda vifijo kelele,nmakofi machezo nderemo
Kusifu kweli kwawapasa,nenyi wanyofu wa moyo
Verse 4
Pigieni Mungu kelele,nimbeni utukufu wake
Tukuzeni sifa za Mungu,ntangazeni matendo yaken
Verse 5
Shukuruni Bwana kwa zeze,nkwa kinanda cha nyuzi kumi
Mfanyieni Bwana shangwe,nmtumikieni kwa furahan