Chorus
Kwa jinsi ujionavyo (ndivyo) ndivyo ulivyoumbwa
Tena kwa mfano wake Yesu Kristu Mwokozi wetu
Furaha leo tuimbe shangwe
Tupige ngoma filimbi na vigelegele
Tufurahi tufurahi na Bwana Yesu
Verse 2
Yeye mwenyewe aliona kwa jinsi hii utapendeza
Sasa mbona wewe wamsahau Bwana Mungu wako
Waisahau hata Sabato siku ya kumshukuru Mungu
Verse 3
Tusijiongeze vitu vingine ndugu vya kujipamba
Njoo kwake Bwana Yesu atakupamba upendeze
Ili uweze kufika kwake Mungu kwenye uzima milele
Verse 4
Ni Yesu Kristu peke yake aliye na upendo zaidi
Katuandalia karamu kabla ya mauti yake
Kaibariki kila tuilapo tupate uzima milele
Verse 5
Ulapo bila kustahili ndugu ungoje hukumu yako
Alisema mwenye moyo safi ajongee mezani
Siku ile ya hukumu nitamwita kwenye ufalme Mbingunin