Kwa Imani Yangu
Ordinary Time,MarianBible Procession
Chorus
(Kwa imani yangu, matendo na maneno
Nihubiri Neno la Mungu siku zote
Nipeleke Neno la Mungu pande zote
Mataifa wanangojea Neno hilo) x2
Verse 2
Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu
Kwa ajili ya uzuri wake wa daima
Uzuri wake Yesu usio na kiasi
Nitende yote mema nifanane na Yesu.
Verse 3
Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu
Nimeyasahau maneno ya zamani
Ya kale yamepita shetani ameshindwa
Nimempata Yesu natembea na yeye
Verse 4
Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu
Kwa ajili ya uzuri wake wa daima
Nakaza mwendo sana nipeleke ujumbe
Ujumbe wake Yesu kwa mataifa yote
Verse 5
Kwa imani pia matendo na maneno
Kwa upendo pia upole na pia nafsi
Nimeweka msingi imara kwake Yesu
Usiotingizika daima siku zote