Chorus
Kusanyikeni kusanyikeni viumbe wake Bwana
Tumsifuni Mungu wetu mwema aliyeumba vyote *2
Amsheni vinanda leteni na zeze na nyimbo nzuri
Zenye kupendeza msifuni Mungu*2
Verse 2
Kaumba nchi, kaumba wanyama,
Binadamu na fikira zake
Lipi lisilomtegemea yeye iwe mvua ama ni jua
Verse 3
Kawapa wengine mali nyingi sana,
Wengine ni dhiki tupu
Ili wote wategemeane kwa kile alichowajalia